Zaidi ya watu 260 wamefariki dunia na 1,000 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha treni tatu katika jimbo la Odisha Mashariki mwa India usiku wa kuamkia leo.
Inadaiwa treni moja ya abiria iliacha njia hadi kwenye njia iliyo karibu na kugongwa na treni nyingine, pia ikagonga treni ya mizigo iliyokuwa imesimama karibu.
Kwa mujibu wa maafisa, Idadi ya vifo inahofiwa kuongezeka huku zaidi ya magari 200 ya kubebea wagonjwa na mamia ya madaktari, wauguzi na waokoaji wakitumwa eneo la tukio.
Inaelezwa kuwa, katika historia ya reli ya India, hii ni ajali mbaya zaidi ya treni kuwahi kutokea katika karne hii.