Watu 8 wakamatwa kwa tuhuma za kumuua Mgambo Kilimanjaro

0
58

Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu nane kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Farijara Hamis Mboya, maarufu kwa jina la Kotex (40), mkazi wa Bomambuzi Manispaa ya Moshi ambaye ni askari mgambo aliyekuwa akisimamia utozaji ushuru katika kituo cha bajaji Mbuyuni.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Simon Maigwa amesema baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa, lilifika eneo la tukio na kukuta mwili ukiwa umelala chini ukiwa na majeraha ya kupigwa na kitu butu kichwani na sehemu mbalimbali za mwili wake.

Amesema tukio hilo limetokea wakati marehemu alipokuwa akirejea kutoka kwenye shughuli zake, na ndipo aliposhambuliwa na watu waliomtuhumu kuwa ni mwizi.

Maigwa amesema mara baada ya uchunguzi kukamilika, wale wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo watafikishwa mahakamani.

Send this to a friend