Watu milioni 250 hatarini kukumbwa na njaa duniani

0
31

Mfumo wa chakuka duniani umeathirika kwa kiasi kikubwa na kuwaweka takribani watu milioni 250 katika hatari ya kukumbwa na njaa, hali inayoweza kuzuilika endapo tu nchi zitashirikiana.

Tishio hilo linatokana na vita ya Urusi na Ukraine, wazalishaji wakubwa ambao wanasambaza asilimia 28 ya ngano duniani, asilimia 29 ya shayiri, asilimia 15 ya mahindi na asilimia 75 ya mafuta ya alizeti.

Vita hiyo si tu imeathiri uzalishaji, bali pia usambazaji wa bidhaa hizo muhimu kutokana kifungwa au kutokufanya kazi kwa ufanisi kwa barabara, bandari na viwanja vya ndege.

Rais wa Urusi, Vladmir Putin amenyooshewa kidole na kuonywa kutotumia chakula kama silaha, kwamba matendo yake yataathiri maisha ya watu kwenye maeneo mbalimbali duniani kwa kiwango ambacho atajutia.

Send this to a friend