Watu sita wakamatwa kwa tuhuma za mauaji ya rapa AKA

0
49

Polisi nchini Afrika Kusini inawashikilia washukiwa sita wa mauaji ya mwanamuziki maarufu, Kiernan Forbes, maarufu kwa jina la AKA, pamoja na rafiki yake wa karibu, Tebello “Tibz” Motshoane waliouawa kwa kupigwa risasi mjini Durban mwaka jana.

Kamishna wa Polisi wa jimbo la KwaZulu-Natal, Nhlanhla Mkhwanazi ameviambia vyombo vya habari kuwa baadhi ya waliokamatwa walikuwa wanahusishwa na kesi za mauaji tofauti, na wawili kati yao walikuwa wamezuiliwa nchi jirani ya Eswatini ambao kwa pamoja walilipwa ili kumlenga AKA.

Mkuu wa Kitengo cha Fedha Serengeti akamatwa madai ya wizi wa milioni 213

“Ilikuwa wazi kwamba AKA alifuatiliwa kutoka uwanja wa ndege na Tibz hakuwa mlengwa aliyekusudiwa katika mauaji kwenye Barabara ya Florida huko Durban,” ameeleza Luteni Jenerali Mkhwanazi.

Aidha, washukiwa hao wote wenye umri wa chini ya miaka 36, wanatazamiwa kufikishwa mahakamani siku ya Alhamisi.

Send this to a friend