Watu wawili hufariki dunia kila dakika kwa ajali za barabarani

0
53

Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zimeonyesha kuwa ajali za barabarani duniani kote zinachukua maisha ya watu takribani milioni 1.3 kila mwaka, ikiwa ni sawa na zaidi ya watu wawili kila dakika huku watu milioni 50 wakijeruhiwa.

Takwimu zimeonesha zaidi ya asilimia 90 ya vifo hivyo vinatokea katika nchi zenye kipato cha chini na kati, na kifo kimoja kati ya vinne vinavyotokana na ajali hizo za barabarani vinawahusu watembea kwa miguu na waendesha baiskeli.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ni muhimu kudumisha usalama wa barabarani kwa kuwa unamuathiri kila mtu.

“Kila siku tunatoka majumbani mwetu kupitia barabara zinazotupeleka kwenye kazi zetu, shuleni na kukidhi mahitaji yetu muhimu ya kila siku. Hata hivyo mifumo yetu ya usafiri inasalia kuwa hatari sana. Hakuna kifo kinachopaswa kukubalika kwenye barabara zetu,” amesema.

Ameongeza kuwa suala la usalama barabarani linahitaji uongozi wa mabadiliko kutoka ngazi za juu za Serikali kuchukua hatua kuhusu azimio la kisiasa lenye lengo la kupunguza vifo na majeruhi wa ajali za barabarani kwa asilimia 50 ifikapo 2030.

Send this to a friend