Watuhumiwa 15 mbaroni kwa mauaji ya wafugaji Tunduma

0
42

Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Kupambana na Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini linawashikilia watuhumiwa 15 waliohusika katika tukio la mauaji ya wafugaji katika kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.

Hayo ya mesemwa leo Septemba 24, 2022 na Kamanda wa Polisi kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo na Migogoro ya Wakulima na Wafugaji nchini, Kamishina Msaidizi wa Polisi, ACP Simon Pasua alipofika Kijiji cha Mbatamila Wilaya Tunduru Mkoa wa Ruvuma na kuwataka wote waliohusika na mauaji hayo wajisalimishe polisi.

Atakayebadilisha, kufichua taarifa binafsi faini milioni 10

Aidha, amewataka wakulima na wafugaji kutojichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate misingi ya sheria na taratibu katika kutatua changamoto zilizopo.

Sambamba na hilo, amewapa pole wananchi waliopoteza ndugu zao na kuahidi kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka watuhumiwa waliobaki ili wafikishwe katika vyombo vya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.

Mbali na hayo, Kamanda Pasua amesema Jeshi hilo limefanikiwa kukamata mifugo 159 iliyokuwa imeibwa katika Kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ambapo amesema Jeshi hilo linaendelea kushirikiana na wafugaji na wakulima katika kupambana na uhalifu wowote ule.

Send this to a friend