Watuhumiwa 210 wa uhaini wafutiwa mashtaka na kuachiwa huru

Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) amewafutia kesi na kuwaachia huru jumla ya washtakiwa 210 waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhaini.
Katika nyakati tofauti, washtakiwa hao wameachiwa katika Mahakama za Mkoa wa Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.
Mkoani Mwanza leo, jumla ya watuhumiwa 139 wameachiliwa katika Mahakama ya Ilemela na Nyamagana, Dar es Salaam wakiachiliwa watuhumiwa 47 huku Arusha wakiachiliwa watuhumiwa 24.
Watuhumiwa hao wameachiwa kufuatia agizo la Rais Samia Suluhu alilolitoa wakati akizindua Bunge la 13 mkoani Dodoma, ambapo alimwagiza Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwasamehe vijana waliofanya makosa kwa kufuata mkumbo.







