Watuhumiwa wa uhujumu uchumi waachiwa kwa dhamana, Waziri Bashe ahoji
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amehoji juu ya kuachiwa kwa dhamana watu waliokamatwa wakivusha mbolea ya ruzuku nje ya nchi wakati wametenda kosa la uhujumu uchumi huku akina mama waliokamatwa wanasafisha kilo 3 za utumbo wakihukumiwa faini ya TZS 300,000.
Waziri Bashe ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 5, 2023 wakati akipokea taarifa ya Mkoa wa Songwe ambapo inadaiwa mawakala waliokamatwa wakivusha mbolea ya ruzuku kwenda nje ya nchi wako nje kwa dhamana.
LATRA: Hakuna mwananchi atakayeshindwa kulipa ongezeko la nauli
“Mimi siyo Jaji wala IGP na si Waziri wa mambo ya ndani lakini kitendo cha Wakala kudanganya mfumo na kunipatia mbolea ya ruzuku ambayo ni kodi za wananchi ni uhujumu uchumi, inakuwaje wapo nje huku naambiwa wanawake waliokutwa wakiosha kilo 3 za utumbo mtoni wakitozwa faini,” amesema Bashe.
Aidha, ameagiza kamati ya ulinzi na usalama mkoani hapo kukutana ili kuona hatua ya kufanya ambayo itafanya watu wengine kutofanya kosa kama hilo.