Watumiaji wa Dawa za Kuongeza Nguvu za Kiume Hatarini Kupoteza Maisha

0
46

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dk Adam Fimbo amewatahadharisha watumiaji wa dawa za kuongeza nguvu za kiume kuwa wapo katika hatari kubwa ya kupoteza maisha kwa kuwa dawa hizo hupanua mishipa ya damu.

Dkt. Fimbo amesema kuwa dawa za kuongeza nguvu za kiume kwasasa zinaongoza zaidi kununuliwa na kutumiwa na wanaume wengi bila kujua kuwa dawa hizo zina madhara makubwa yatakayopelekea kupoteza maisha yao.

“Watumiaji wa dawa hizi watakufa kwa sababu zinapanua mishipa ya damu, mishipa ya kichwani ikishapanuka, itapasuka na hivyo mtumiaji wa dawa hizi atakufa tu.” amesema Dkt. Fimbo.

Send this to a friend