Watumiaji wenye ‘blue tick’ Facebook na Instagram kuanza kulipia  

0
44

Kampuni ya Meta imetangaza kuwa watumiaji wa Instagram na Facebook sasa wataweza kulipia ili akaunti zao zithibitishwe (verification).

Ulipiaji huo umethibitishwa kugharimu $11.99 (TZS 28,000)) kwa mwezi kwenye wavuti, au $14.99 (TZS 35,000) kwa watumiaji wa iPhone.

Mark Zuckerberg, Mtendaji Mkuu wa Meta, amesema hatua hiyo itaboresha usalama na uhalisi kwenye programu za mitandao ya kijamii.

Hatua hiyo inajiri baada ya Elon Musk, mmiliki wa Twitter, kutekeleza mfumo wa uthibitishaji wa kulipia kuanzia Novemba 2022.

“Usajili huo utawapa watumiaji wanaolipa ‘blue tick’ mwonekano zaidi wa machapisho yao, ulinzi dhidi ya waigaji na ufikiaji rahisi wa huduma kwa wateja,” Meta imeandika kwenye tovuti yao.

Mambo ya msingi ya kufahamu unapotaka ku-verify akaunti ya Twitter

Kampuni hiyo imeiambia BBC kuwa mabadiliko hayo hayataathiri akaunti zilizoidhinishwa hapo awali, lakini ikabaini kuwa kutakuwa na ongezeko la kuonekana kwa baadhi ya watumiaji wadogo ambao watathibitishwa kutokana na kipengele cha kulipia.

Meta imesema majina ya watumiaji ya Instagram na Facebook yatalazimika kuendana na hati ya kitambulisho iliyotolewa na serikali ili kupata uthibitisho, na watumiaji watalazimika kuwa na picha ya wasifu inayojumuisha sura zao.

 

 

Send this to a friend