Watumishi saba Liwale kuadhibiwa kwa kutotimiza wajibu wao

0
28

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Miko na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, amemuelekeza Katibu Mkuu kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi saba wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale mkoani Lindi kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Akiwa ziarani mkoani humo, Waziri Mchengerwa ameelekeza hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa mujibu wa Kanuni ya 42 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2022, inayoainisha kuwashusha vyeo, kukatwa mshahara kwa asilimia 15 kwa muda usiopungua miaka 3 pamoja na kufukuzwa kazi iwapo watabainika kufanya makosa hayo.

Watumishi wanaotakiwa kuchukuliwa hatua hizo za kinidhamu ni; Kaimu Mhandisi wa Wilaya (Sisty Njau), Mkuu wa Idara ya Maliasili (Damasi Mumwi), Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika (Mustafa Magembe), Mkuu wa Idara ya Ugavi na Ununuzi (Vinsent Moyo), Mkuu wa Idara ya TEHAMA (Mohamedi Songolo), Katibu wa Afya (Sadick Bakari Khatibu), Afisa Ugavi na Ununuzi aliyehamishiwa Halmashauri ya Wilaya Kilwa (Tunu Mtamaha).

Wasira: Viongozi wa dini achaneni na siasa, hubirini amani

Mbali na hayo, Waziri Mchengerwa ameelekeza kuwa kuanzia sasa maofisa wote wenye kesi za rushwa na ubadhirifu wasihamishwe vituo vyao vya kazi mpaka mashauri yao yanapokamilika.

Send this to a friend