Mamia ya watumishi wa umma wa sekta ya afya nchini Zimbabwe wamegoma kutoa huduma kutokana na mishahara kuwa midogo na mazingira duni ya kazi.
Hali hiyo iliyochangiwa na hali mbaya ya kiuchumi imepelekea maelfu ya wafanyikazi wa afya kuacha utumishi wa umma katika miaka mitatu iliyopita.
Aidha, viongozi wa vyama vya wafanyakazi wamekiri kwamba wagonjwa wanaweza kufa kutokana na mgomo huo, lakini wamedai hawawezi kulisha familia zao.
Awali, Serikali ilisema itaongeza mishahara maradufu mwezi Julai, lakini Afisa wa Chama cha Wafanyakazi ameripoti kuwa kiasi kilichopendekezwa bado hakitakidhi mahitaji yao.
Gharama ya chakula na huduma imeongezeka zaidi ya mara mbili hivi karibuni kutokana na vita vya Ukraine na mfumuko wa bei wa kila mwaka ukifikia zaidi ya asilimia 130 mwezi Mei.