Watumishi Tanga wasimamishwa kazi kwa kuchelewa kufika eneo la ajali

0
58

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amewasimamisha kazi watumishi wa umma wawili ili kupisha uchunguzi wa sababu za kuchelewa kufika katika eneo la tukio baada ya ajali kutokea wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Ametoa agizo hilo Mgumba wilayani Korogwe baada ya kuzungumza kwa undani na watumishi pamoja na ndugu wa marehemu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

Watu 17 wafariki ajalini Tanga wakisafirisha maiti

Watumishi waliosimamishwa kazi ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Salma Swedi na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Magunga, Korogwe Dkt. Heri Kiwale.

Ajali hiyo ilitokea Februari 03, 2023 majira ya saa 4 na nusu usiku, huku watumishi wa hospitali hiyo wakifika eneo la tukio saa kumi kasoro alfajiri hii leo.

Send this to a friend