Watumishi wa afya walioonekana wakibishana wasimamishwa kazi

0
39

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Uyuwi, Dkt. Kija Maige amemsimamisha kazi Muuguzi Mkunga, Rose Shirima na Mtekenolojia wa Maabara, James Getogo wa Zahanati ya Ishihimulwa  ili kupisha uchunguzi.

Watumishi hao wa afya wameonekana katika video inayosambaa mitandaoni wakibishana huku mmoja akipinga kutumia vitendanishi vilivyoisha muda wa matumizi.

Aidha, Dkt. Maige amesema  uchunguzi huo utashirikisha mabaraza yao ya kitaaluma ambayo ni Baraza la Wauguzi Tanzania na Baraza la Wataalam wa Maabara Tanzania na hatua zaidi zitafuatwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo.

Send this to a friend