Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko amewasimamisha kazi baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Ugalla kilichopo Kata ya Ugalla Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi baada ya kushindwa kufanya usafi katika maeneo ya hospitali.
Watumishi hao wamesimamishwa kazi leo Februari 16, 2024, ili kupisha uchunguzi kutokana na uzembe walioufanya wa kukitelekeza kituo hicho baada ya kufanya ziara na kukuta hali isiyoridhisha katika kituo hicho ambacho kimejaa nyasi na kutopata majibu ya kuridhisha.
Waliosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Nsimbo, Ofisa Manunuzi, Ofisa Tarafa, Mtendaji wa Kata ya Ugalla, Mtendaji wa Kijiji, na wengine watakaobainika kuhusika.
P2 inavyoweza kusababisha madhara kwenye hedhi na mifupa
“Mmenileta hapa ili nipongeze kwamba mnafanya kazi nzuri? au mlitegemea hapa mimi nije nifanye nini? na sasa hivi mnasema tupe masaa sijui mangapi tufanye usafi, wanini? wananchi wanaokaa huku ndiyo wanapaswa wafanyiwe usafi sio usafi ufanywe kwa ajili yangu mimi,” amesema Mrindoko.
Aidha, amesema sio sahihi kwa wananchi wanaoishi eneo hilo kukutana na nyasi katika kituo hicho cha afya kilichofanywa nyumba ya wadudu kama mchwa na wengine.
Chanzo: Habari Leo