Watumishi wa afya wasimamishwa kazi tukio la watoto njiti kung’olewa macho

0
56

Kufuatia tukio la vifo vya mapacha wawili njiti waliodaiwa kuuawa huku wakinyofolewa macho, kuchunwa ngozi ya paji la uso na kukatwa ulimi  mara baada ya kuzaliwa katika hospitali ya Kaliua mkoani Tabora, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema watumishi waliohusika wamesimamishwa kazi.

Akiandika kupitia ukurasa wake wa twitter, Waziri Ummy amesema uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa jambo hilo ni la kweli na kumuagiza RMO wa Tabora kusimamia vyema weledi, maadili na miiko ya watumishi wa afya.

“Tumelifuatilia suala hili, kuna ukweli. Uongozi wa (W) Kaliua umeshaanza kuchukua hatua. Baadhi ya Watumishi wa Afya waliomuhudumia mama huyu wameshasimamishwa kazi. Nakemea vikali kitendo hiki. Ninamuagiza RMO Tabora kusimamia vyema weledi,maadili na miiko ya watumishi wa afya,” amesema.

Serikali yatangaza jina jipya la Hospitali ya Mirembe

Kupitia mtandao wa Facebook, anayedaiwa kuwa baba mzazi wa mapacha hao, Kisaka Mtoisenga amesema watoto walizaliwa salama licha ya kuwa njiti, na kwa kuwa kituo hicho hakina uwezo wa kuhudumia watoto njiti, kituo kiliwapa rufaa kwenda hospitali teule ya Wilaya na kuwashauri watafute usafiri binafsi kwani kituo hakina gari la wagonjwa.

Ameongeza kuwa baada ya kupata usafiri, wahudumu waliwaomba wasubiri kwani bado wanawaandaa watoto, kisha baada ya muda wahudumu walitoka na kuwaeleza kuwa tayari wamefariki na kwamba watawapa miili hiyo asubuhi.

“Asubuhi wakatupatia maiti zikiwa ndani ya maboksi, kwenye chumba maalum cha upasuaji ambacho kuna giza. Wakatusisitiza tukazike siku hiyo hiyo kwa haraka kwa sababu watoto njiti hawafanyiwi msiba, kabla ya kupanda gari.

Tukaenda polisi, lakini wakatuambia tukazike tu maana hawashughuliki na ushirikina. Tukaenda kwa Mkuu wa Wilaya, alipoona maiti akasema huo ni ushirikina, akatushauri tukazike tu,” ameeleza.

Send this to a friend