Watumishi wa bandari watakiwa kuchagua kati ya TPA au DP World

0
35

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesema kutokana na mabadiliko ya uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, watumishi wa bandari hiyo wametakiwa kuchagua endapo watabakia TPA au kusitisha mkataba wa ajira na TPA na kuajiriwa na DP World papo hapo.

TPA imesema taarifa hiyo ilitolewa kwa watumishi wake Machi 20, 2024 juu ya mabadiliko hayo yanayotokana na mabadiliko ya mkataba kati ya TPA na kampuni ya DP World ya Dubai kuhusu uendeshaji na uendelezaji wa Gati namba 0-7 za Bandari ya Dar es Salaam kwa kipindi cha miaka 30 kuanzia Oktoba 22, 2023.

“Menejimenti ya TPA ilitoa taarifa hiyo kwa watumishi baada ya kukamilisha programu maalum ya kuwaelimisha na kutoa ufafanuzi wa kina na taarifa sahihi kuhusiana na mabadiliko tajwa kwa watumishi wake,” imeeleza taarifa.

Bunge lakanusha wabunge kuongezewa mishahara hadi milioni 18

Aidha, TPA imesema taarifa iliyotolewa na Menejimenti ilielekeza watumishi watakaoridhia kujiunga na DP World kwa hiari yao kuwasilisha taarifa zao katika makao makuu ya TPA kabla au ifikapo Machi 29, mwaka huu.

Vilevile, kwa watumishi ambao hawatopenda kujiunga na DP World watabaki TPA kwakuwa mamlaka hiyo itaendelea kuhitaji watumishi watakaotoa huduma katika bandari zake zinazoendelea kuboreshwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Send this to a friend