Watumishi wa Serikali wadaiwa kwenda baa na nyaraka za Serikali

0
42

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde amekemea tabia ya baadhi ya watumishi kwenda na nyaraka za Serikali katika maeneo ya baa na majumbani, jambo linalopelekea kuvuja kwa siri za Serikali.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu Tawala na Wakuu wa Idara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa jijini Dodoma, ambapo ameeleza kuwa bado kuna tatizo la baadhi ya watumishi kutokutunza nyaraka za Serikali huku wengine wakitembea na majalada ya siri yakiwa hayajafunikwa.

Orodha ya majina ya vijana 812 waliochaguliwa kujiunga na programu ya kilimo (BBT)

“Wengine wanakwenda na nyaraka za Serikali nyumbani na wengine wanatoa taarifa kuhusu nyaraka au jambo fulani kwenye baa. Hali hii inasababisha usalama wa nyaraka za Serikali kutozingatiwa, na hivyo kuhatarisha ustawi wa taifa,” amesema Silinde.

Aidha, amewaagiza watumishi kudhibiti uvujaji wa siri za Serikali katika zama hizi za utandawazi na mitandao ya kijamii ili kuongeza uadilifu katika utumishi wa umma kwani siri hizo ndio uhai wa Serikali.

Send this to a friend