Watumishi wanne wafukuzwa kazi kwa ubadhirifu wa fedha

0
39

Watumishi wanne katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete wamefukuzwa kazi kwa ubadhirifu wa fedha za mapato ya ndani na mmoja akifukuzwa kwa utoro kazini na kuisababishia hasara Serikali.

Maamuzi hayo ni kufuatia kikao maalumu cha baraza la madiwani kilichokutana kujadili maadili ya watumishi zaidi ya 60 ambapo kati ya hao, watumishi wanne wamefutwa kazi na watumishi watano watakatwa mishahara yao kwa asilimia 15 kwa mwaka mmoja, wengine miaka miwili na mmoja miaka mitatu.

Watumishi waliofukuzwa ni aliyekuwa Mtendaji Kata ya Mbalatse, Omega Aloyce Thobias ambaye amefukuzwa kwa utoro kazini kwa kipindi cha siku 214, waliokuwa watendaji wa vijiji Bryson Isaack Sanga aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Ludihani, Godwin Jacob Luvanda aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Ikuwo na Tumaini Shem Ngogo, Mtendaji wa Kijiji cha Kigala.

Watendaji hao watatu wamefukuzwa kwa ubadhirifu wa fedha za mapato ya ndani ambapo Tumaini Ngogo amekusanya fedha zaidi ya shilingi milioni 44 na kutopeleka benki.

Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya Kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe amesema kufuatia kubainika na makosa, watumishi hao wamefutwa kazi kuanzia sasa.

Send this to a friend