Watumishi wasiokwenda likizo wanaiibia Serikali

0
43

Ofisa Utumishi wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Fortunatus Mabula amewaonya watumishi kuacha tabia ya kutokwenda likizo kwani kwa kufanya hivyo ni kuiibia serikali.

Ameyasema hayo mkoani humo wakati wa kikao kazi kilichoandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) ambapo amesema baadhi ya watumishi wamejijengea utaratibu wa kutokwenda likizo na uchelewaji kazini akisisitiza kuwa ni ukosefu wa nidhamu kiutumishi.

Aidha, Mabula amesema Serikali iliagiza mfanyakazi anapostaafu atalipwa pensheni ya asilimia 33 ambayo atalipwa kwa mkupuo, kisha atapokea asilimia 67 iliyobaki kila mwezi.

Hata hivyo amewakumbusha watumishi kuwa wanapodai haki zao kutoka kwa waajiri wakumbuke kutimiza wajibu na majukumu yao kutokana na miongozo ya kazi walizopewa.

Send this to a friend