Wauguzi wasimamishwa kazi baada ya mtoto kuharibika mkono

0
68

Wizara ya Afya Zanzibar imewasimamisha kazi wauguzi wawili kutoka Hospitali ya Mkoa Lumumba kupisha uchunguzi kufuatia tukio la mtoto wa miezi minne kuharibika mkono kwa madai ya uzembe wa baadhi ya wauguzi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Mngereza Miraji amesema baada ya kupokea malalamiko yaliyotolewa na wazazi wa mtoto huyo, walifanya uchunguzi kubaini chanzo pamoja na hatua za kufuata.

Amesema mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo Novemba 15, 2025 na kupatiwa huduma ya upasuaji wa tumbo uliosababishwa na utumbo mdogo na mkubwa kuingiliana, ambapo upasuaji huo ulifanikiwa.

Wakati matibabu yakiendelea ndipo mkono wa mtoto ulianza kuvimba na kubadilika rangi, hali iliyopelekea asafirishwe kwenda Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

Chanzo: Nipashe

Send this to a friend