Wawili wakutwa wameungua moto kwenye msitu wa hifadhi Korogwe

0
102

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limesema watu watatu wamefariki dunia baada ya kuungua moto katika eneo la ndani ya Msitu wa Hifadhi ya Korogwe Fuel katika Kijiji cha Sindeni wilayani Handeni mkoani humo.

Kamanda wa Polisi, Almachius Mchunguzi amesema walipokea taarifa ya ajali hiyo
Septemba 23, mwaka huu majira ya saa 03:45 usiku, na baada ya uchunguzi wa awali wa miili iliyokuwa nje ya gari ilibainika ni ya jinsia ya kike na ndani ya gari kiti cha nyuma ulionekana mwili mwingine ambao umeuungua moto hadi kutotambulika ambao haukubainika ni wa jinsia gani.

“Askari Polisi walifika eneo hilo na kukuta kweli kuna gari aina ya IST lenye namba T T 305 EAL linaungua moto na pambeni yake kukiwa na watu wawili wameungua kwa moto,”amesema Kamanda Mchunguzi.

Miili ya watu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Handeni huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya uchunguzi ili kubaini watu hao walioteketea kwa moto ni akina nani , na nini kiliwatokea kabla ya umauti na waliofanya tukio hilo ni watu gani ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Send this to a friend