Wawili washikiliwa kwa mauaji Arusha

0
68

Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za kumuua Israel Paulo (36), Mkulima na Mkazi wa Leguruki, Wilaya ya Arumeru mkoani humo kwa kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Justine Masejo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Ndewario Lazaro maarufu kwa jina Shombotoni (60), Mkulima na Mkazi wa Mwaruvango Wilaya ya Arumeru, na Oscar Ndewario (29), mkazi wa Moivaro ambaye alitoroka baada ya tukio na baadaye kukamatwa Wilaya Simanjiro Mkoani Manyara.

Jeshi la Polisi kuchunguza vifo vya watoto mapacha Tegeta

Kamanda Masejo amesema kuwa jeshi hilo linaendelea na upelelezi ambapo jalada litafikishwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka mara baada ya upelelezi huo kukamilika.

Aidha, Jeshi la Polisi limewashukuru wananchi kwa ushirikiano na jeshi hilo katika kufichua matukio ya uhalifu na kuwaomba wananchi kufuata sheria na kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Send this to a friend