Wazazi jela maisha kwa kumuua binti yao aliyekataa kuolewa na binamu yake

0
51

Mahakama nchini Italia imewahukumu wazazi wawili wa Kipalestina, Shabbar Abbas na Nazia Shaheen kifungo cha maisha jela kwa kumuua binti yao, Saman Abbas mwenye umri wa miaka 18 baada ya kukataa kusafiri kwenda Pakistan kwa ajili ya ndoa iliyopangwa.

Mwezi wa Novemba mwaka jana, mwili wa Saman Abbas uligunduliwa katika shamba karibu na eneo la kazi la baba yake kaskazini mwa Italia baada ya kutoweka mwezi Aprili 2021.

Katika chapisho moja kwenye mitandao ya kijamii, binti huyo na mpenzi wake walionekana wakibusiana barabarani hivyo kulingana na uchunguzi uliofanywa, picha hiyo iliwakasirisha wazazi wake ambao walitaka yeye aolewe na binamu yake nchini Pakistan.

Njia 10 za kumwelewa mwanamke

Uchunguzi wa maiti ulionyesha shingo ya msichana huyo ilikuwa imevunjika katika kile kilichotafsiriwa ni kutokana na kunyogwa au kubanwa.

Mjomba wake, Danish Hasnain amehukumiwa kifungo cha miaka 14 gerezani, kwa kuhusika katika mauaji hayo huku baba wa Abbas, akidai hana hatia juu ya mashitaka hayo na pia anataka kumjua muuaji wa binti yake.

Inasemekana Abbas alimwambia mpenzi wake kwamba alikuwa akihofia maisha yake kutokana na kukataa kwake kuolewa na mwanaume aliyemzidi umri katika nchi yake ya Pakistan.

Send this to a friend