Wazazi wagundua mtoto wao amefariki siku ya pili

0
37

Mtoto Esanto Mtewa (7) kutoka Kijiji cha Utilili wilayani Ludewa mkoani Njombe amefariki baada ya kudondokewa na ukuta wa boma la nyumba huku wazazi wakigundua kifo cha mtoto wao siku ya pili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah amesema tukio hilo limetokea Novemba 10 jioni alipokuwa akirudi shule wakati huo mvua kubwa ilikuwa ikinyesha iliyoambatana na upepo. Mtoto huyo alikuta mlango umefungwa hivyo kuamua kujikinga kwenye boma hilo na ndipo ulipomuangukia na kusababisha kifo chake.

Waganga waonywa kuwapa watoto dawa za mvuto wa kimapenzi

Kamanda ameeleza kuwa wazazi wa mtoto huyo waliporudi walilala mpaka asubuhi bila ya kuangalia iwapo mtoto wao yuko ndani au la, na walipomtafuta baadaye waliona ukuta umeanguka huku mguu wa mtoto ukiwa umetokeza na ndipo walipobaini kuwa ni mtoto wao.

“Wazazi ambao mnaweza mkaingia ndani mkalala bila ya kujua watoto wamelalaje, hii ni namna fulani ya kauzembe, wazazi msiwe na hiyo hali ya kuwasahau watoto, kwetu sisi huu uzembe tunasema ni ukatili. Kwahiyo tunawaomba msiwe na hiyo hali ya ukatili, muwalinde watoto,” amesema.

Send this to a friend