Wazazi wamshtaki kijana wao kwa kutowapatia mjukuu

1
40

Wanandoa katika Jimbo la Uttarakhand, Kaskazini mwa India, Sanjeev (61) na Sadhana Prasad (57) wamemshtaki kijana wao wa pekee na mkewe kwa kutowapa mjukuu baada ya miaka sita ya ndoa yao.

Wanandoa hao wamedai kwamba walitumia akiba yao kumlea mtoto wao wa kiume, kumlipia mafunzo ya urubani, kugharamikia harusi yake katika hoteli ya nyota tano pamoja na gari la kifahari lenye thamani ya dola 80,000 (sawa na TZS 186,000,000) kisha kuwapeleka kwenye fungate nje ya nchi.

“Mwanangu amekuwa kwenye ndoa kwa miaka sita lakini bado hawajapanga kupata mtoto, angalau ikiwa tuna mjukuu wa kukaa naye, maumivu yetu yatavumilika,” Prasad amesema.

Hata hivyo, wamedai fidia ya thamani ya karibu $ 650,000 (sawa na TZS 1,511,250,000) ikiwa hakuna mjukuu atakayezaliwa ndani ya mwaka mmoja.

Ombi la wanandoa hao lililowasilishwa mahakamani linatarajiwa kusikilizwa Mei 17, ingawa kijana wake na mkewe hawaonekani kutoa maoni yoyote kuhusu hilo.

Send this to a friend