Wazazi wanaosambaza video za watoto mitandaoni waonywa

0
58

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amewataka wazazi kuacha mara moja tabia ya kuweka picha na video za watoto kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonesha wakiimba na kucheza kwani vitendo hivyo havileti mafundisho mazuri kwa watoto.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto mkoani humo ambapo amesema kitendo cha kuwarekodi watoto na kusambaza video zao kimekuwa kikimuumiza kama mzazi, kwani baadhi ya nyimbo wanazoimba watoto hao haziendani na umri wao, na zinaweza kuleta athari baadaye.

Chuo chawekwa chini ya uangalizi kwa kutoa programu iliyofutwa

Aidha, Kunenge amesema ni lazima wazazi na walezi wawe karibu na watoto ili kufuatilia maendeleo yao sambamba na kuwakagua mara kwa mara masomo yao na kazi za darasani badala ya kuwaachia wasaidizi wa kazi.

Send this to a friend