Wazazi watakaokaidi chanjo ya polio kutozwa faini

0
30

Wananchi wametakiwa kuwatoa watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano kupata chanjo ya Polio awamu ya tatu, na kwa wale watakaokaidi watachukuliwa hatua za kisheria.

Hayo yamebainishwa na Mwanasheria wa Manispaa ya Kahama, Stephen Magala alipokuwa kwenye kikao kazi cha Kamati ya Afya ya Msingi mkoani Shinyanga.

Magala amesema, “kwa mzazi au mlezi atakayekaidi kumtoa mtoto kwa ajili ya chanjo ya polio, atatozwa faini ya TZS 100,000 au kwenda jela miezi mitatu au vyote kwa pamoja.”

TMA yatoa tahadhari kipindi cha vuli

Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Msalala, Peter Mlacha amesema watoto ambao hawatofikiwa kwa awamu hii na kupatiwa chanjo, watalazimika kufika kwenye vituo vya afya jirani na makazi yao, kwakuwa huduma hiyo imeendelea kutolewa kwenye vituo vya afya ngazi ya jamii.

Chanjo ya Polio imeanza kutolewa hapo juzi na itadumu ndani ya siku nne ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa sheria ya afya ya jamii.

Send this to a friend