Wazazi watelekeza watoto, Baba aoa na mama aolewa na mtu mwingine

0
14

Mkuu wa Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, Ngollo Malenya ameliagiza Jeshi la Polisi wilayani humo kuwasaka na kuwakamata Thomas Ulanda pamoja na aliyekuwa mkewe Adelyda Nakashawa kwa kuwatelekeza watoto wao watatu.

Agizo hilo limekuja baada ya taarifa kuwa wazazi hao waliwatelekeza watoto wao mbao wote ni wa kike tangu mwaka 2017 katika Kijiji cha Gombe, wilayani humo, baada ya mzazi wa kiume kuoa mwanamke mwingine na mzazi wa kike kuolewa na mwanaume mwingine.

Maambukizi ya UVIKO-19 yaongezeka nchini

Watoto hao wametajwa kuwa ni Elionida Ulanda (17), mwanafunzi kidato cha nne, Christina Ulanda (13), darasa la saba na Sylivia Ulanda (09) anayesoma darasa la pili.

Aidha, Ulanga amesema kwa sasa watoto hao wamepata mdau kutoka kampuni ya uchimbaji wa madini, John De Vries ambaye anawahudumia mahitaji yao chini ya uangalizi wa bibi yao, pia ameanza kuwajengea nyumba ambayo itakuwa chini ya majina yao.

Send this to a friend