Wazazi wawatishia watoto kifo endapo watafaulu mtihani wa darasa la saba

0
55

Baadhi ya wazazi wilayani Makete mkoani Njombe wamedaiwa kuwatisha watoto wao wanaohitimu elimu ya msingi kufanya vibaya kwenye mitihani kwa madai kuwa wakifaulu wao watafariki dunia.

Ameeleza hayo Ofisa Mtendaji wa Kata ya Lupila, Tumwanukye Ngakonda kwamba baada ya wanafunzi hao kuhojiwa kutokana na mabadiliko yao ya kitaaluma kuelekea mitihani yao ya mwisho walidai kushinikizwa kufanya vibaya kwa kuhofia kuwapoteza wazazi wao kwa kigezo kwamba wakifaulu watashindwa kuwasomesha kutokana na hali mbaya ya kiuchumi.

Walimu waongoza kwa utoro kwa asilimia 66.5

“Kwa sababu ya changamoto hiyo Wilaya ya Makete tumejiwekea mikakati ya kusimamia ipasavyo elimu kwa kuhakikisha kila mwanafunzi aliyefaulu anaripoti na kuendelea na masomo ya Sekondari,” amesema Ngakonda.

Ameongeza kuwa baada ya kugundua tatizo hilo wamechukua hatua ikiwa ni pamoja na utoaji elimu kwa wanafunzi kutokubali kufeli na katika elimu hiyo wamekutana na shuhuda mbalimbali ikiwemo wazazi kuwaambia kuwa endapo watafaulu hawatokuwa watoto wao.

Chanzo: Nipashe

Send this to a friend