Wazikaji waandamana Afrika Kusini, wagoma kuzika miili ya watu

0
21

Takribani wazikaji 3,000 wameandamana nchini Afrika Kusini wakitaka kulipwa vizuri pamoja na mazingira mazuri ya kufanya kazi yao.

Wazikaji hao wamegoma kuchukua miili ya watu waliofariki majumbani mwao, hospitali pamoja na kuendesha shughuli za uzikaji wa miili hiyo.

Waandamanaji hao wanaishinikiza serikali kuanzisha mfuko wa virusi vya corona ambao utawapa nafuu kwenye ufanyaji kazi zao.

Gharama ha uzikaji au uchomaji moto wa miili ya watu waliofariki imeongezeka kwa hadi 25% tangu kuanza kwa janga la corona nchini Afrika Kusini. Ongezeko hilo limechangiwa na uhitaji wa mavazi ya kujikinga (PPE), vipukusi (sanitisers) na vifaa kinga vinginevyo.

Mamlaka zimesema kuwa kuna hatari ya mgomo huo ukahatarisha usalama wa afya za watu.

Send this to a friend