Waziri Afya apendekeza Hospitali ya Mirembe ibadilishwe jina

0
23

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amependekeza Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe kubadilishwa jina ili wananchi kujitokeza kwa wingi na kupata huduma katika hospitali hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi Mpya ya Ushauri ya Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe amesema kituo hicho kitahusisha huduma za tiba ya akili, tafiti mbalimbali za maradhi hayo, mafunzo ya Afya za akili na kuhamasisha jamii kuwa na uelewa juu ya Afya ya akili.

“Bodi na wajumbe natamani Mirembe tuiite Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akili, nawaachia mjadili na mniambie kama ni kubadilisha sheria mimi nipeleke kwenye baraza ijadiliwe”, amesisitiza.

Aidha, ameitaka bodi hiyo kujikita katika masuala ya kukuza afya ya akili ikiwa ndiyo lengo mahususi la kuanzishwa kwa hospitali hiyo hapa nchini.

Mkurugenzi aliyedaiwa kuuza viwanja kwa bilioni 1 atumbuliwa

“Nafahamu kwa sababu wagonjwa hawa wa afya ya akili pia hawalipii kwa hiyo madaktari na wenyewe tunajua motisha unatokana na asilimia iliyoingia ya kuona wagonjwa kwa hiyo tujitahidi tufantye lakini tusije tukaathiri utoaji wa huduma kwa ajili ya afya ya akili,” ameongeza.

Amebainisha kuwa maono yake ni kuona Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili Mirembe kuwa kituo cha umahiri cha masuala ya afya ya akili na magonjwa ya akili nchini kitakacholeta matokeo mazuri juu ya tafiti mbalimbali zitakazofanywa.

Send this to a friend