Waziri Aweso awasweka rumande vigogo watano Mwanza

0
42

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuwaweka mahabusu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mjini Mwanza (MWAWASA), Meneja wa Mamlaka ya Maji Vijijini Mkoa wa Mwanza (RUWASA), Meneja wa Maji Vijijini Wilaya ya Sengerema, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Sengerema na Mkandarasi.

Aweso ameagiza Watu hao wawekwe ndani hadi kesho atakapokutana nao ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa maamuzi zaidi.

Amefikia maamuzi hayo baada ya kukutana na changamoto kubwa ya kutokamilika, kutumia pesa kinyume na taratibu na utekelezaji usiokidhi vigezo kwa mradi wa maji tegemezi kwa Wilaya ya Sengerema wa Busurwangiri.

Mradi huo umetumia TZS bilioni 1.8 na lakini bado wananchi hawapati maji hivyo kupelekea kunywa maji ya mashimoni yenye tope.

Send this to a friend