Waziri Bashe: Acheni kilimo cha Twitter na WhatsApp

0
67

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amewatahadharisha Watanzania kuachana na njia za mkato kwenye kilimo ili kuepuka utapeli unaoendelea kupitia mitandao ya kijamii na kwamba Serikali inafuatilia makampuni yanayodaiwa kufanya udanganyifu huo.

Akizungumza leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa taarifa maalum kuhusu ziara za Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Bashe amesema hivi karibuni Serikali imetunga sheria ambapo inaanzisha mamlaka iitwayo ‘Copra’ ambayo itasimamia na kudhibiti shughuli zote za uzalishaji, masoko na biashara kwenye sekta hiyo.

“Acheni kulima kwa Twitter na Whatsup. Hamna mtu anaweza akakuambia leta milioni 10 baada ya miezi mitatu njoo uchukue utapata milioni 15. Niwaombeni ndugu zangu kwenye kilimo hakuna njia ya mkato,” amesema Waziri Bashe.

Serikali yaeleza chanzo cha meli ya Tanzania kuzama nchini Iran

Aidha, Bashe amesema kulingana na takwimu za sasa, takribani watu milioni 800 wapo kwenye hatari ya kukumbwa na janga la njaa, huku akibainisha kuwa mwezi Septemba mwaka huu Tanzania inatarajia kuwa na kiwanda cha kwanza cha mbolea nchini kitakachosaidia wakulima kutekeleza shughuli zao za kilimo.

Send this to a friend