Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kwa sasa Tanzania haipo tayari kutumia mbegu zilizobadilishwa vinasaba (GMO) pasipo kujua undani wake, badala yake itatenga maabara mbili ili kuendelea kujifunza na kupata elimu kuhusu aina hiyo ya mbegu.
Ameyasema hayo katika mkutano na wahariri wa vyombo vya habari pamoja na wadau wa sekta ya kilimo jijini Dodoma kwa ajili ya kuwaelezea utekelezaji wa Agenda 10/30 kilimo biashara.
“Hatutumii GMO, na hatutotumia, labda baadaye sijui baadaye, lakini kwa sasa hatutotumia GMO seeds [mbegu], lakini hatutoacha kujifunza kuhusu GMO [..] Sisi kama nchi hatuwezi kukataa kitu tusichokijua kwamba sisi hatutaki GMO, mtu akikwambia GMO ni nini? Huijui,” amesema Waziri Bashe.
Wakulima wadai baadhi ya mawakala wanaficha mbegu za ruzuku
GMO ni mazao yaliyobadilishwa vinasaba, au mazao yaliyoundwa na vinasaba vilivyofanyiwa uhandisi jeni ambapo inatajwa kuwa na athari kwa binadamu, wanyama na mazingira kwa ujumla.