Waziri Gwajima: Tukio la kupigwa kwa binti Songwe ni la kweli

0
40

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Doroth Gwajima amewaagiza wasidizi wa kisheria kufuatilia kwa ukaribu juu ya tukio la binti Florenencia Mjenda (20) mkazi wa Kata ya Mbangalo wilayani humo anayedaiwa kupigwa na Mkuu wa Wilaya ya Songwe, Simon Simalinga.

Akitoa taarifa hizo leo Desemba 06, 2022 Waziri Gwajima amesema taarifa hizo ni za kweli baada ya kikosi cha Maafisa Ustawi wa Jamii aliowaagiza kufuatilia mkoani Songwe kuthibitisha madai hayo.

“Tukio ni la kweli, binti ana miaka 20 na ameshafungua kesi ya shambulio la aibu Na. Mkw/IR/1149/2022 Polisi Kituo cha Mkwajuni. Nimetuma tena kikosi hicho kiende kijijini nyumbani kwa binti huyu wampe ushauri nasaha wakati shauri likiendelea. Aidha, wasaidizi wa kisheria wafuatilie kwa karibu hatua zote,” ameagiza Gwajima.

Kesi ya Mdee na wenzake yahairishwa hadi Machi 2023

Ameongeza, “binafsi nimesikitishwa na tukio hili, nakemea viongozi kwenda nje ya taratibu na kuanza ugomvi binafsi na wananchi ambapo wanawake, wasichana na watoto wanakuwa wahanga zaidi. Haikubaliki.”

Katika video inayosambaa mtandaoni inamuonesha binti ambaye amedai kushambuliwa na Mkuu huyo wa Wilaya, huku akitaja sababu kuwa ni baada ya yeye na wenzake waliokuwa uwanjani kwa ajili ya michezo kuketi kwenye jukwaa ambalo Mkuu huyo alidai halikuitengenezwa kwa ajili ya watu kukaa.

Send this to a friend