Waziri Kijaji awapa waandishi maelekezo ya habari za kuandika

0
71

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Ashatu Kijaji amewataka waandishi wa habari kuchuja kile wanachokiandika, ili kitakachotoka kiwe ni chenye maslahi kwa nchi.

Dkt. Kijaji amesema kuwa ni lazima kila mmoja ajivunia kuwa Mtanzania, na kwamba akishajivunia ataepuka vishawishi vya kulichafua Taifa.

“Utaepuka vile vishawishi vya kuwafanya Watanzania wasikie wasichotaraji kukisikia. Na kwa hili sitokuwa na uvumilivu,” amesisitiza.

Amesema watasimamia maadili kuhakikisha kuwa Taifa linapata taarifa zile zinazohitaji tu.

Septemba 12 mwaka huu Rais Samia Suluhu Hassan alimteua Dkt. Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akichukua nafasi ya Dkt. Faustine Ndugulile ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Send this to a friend