Waziri Makamba aitaka TANESCO kutokodi mitambo ya dharura ya kuzalisha umeme

0
25

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Serikali zinachukua hatua za muda mfupi, wa kati na muda mrefu kukabiliana na upungufu wa umeme ulipo nchini kwa sasa.

Amesema hayo akiwa katika doria kwenye mito inayoingiza maji katika mabwawa ya vituo vyote vya kuzalisha umeme kwa nguvu ya maji.

Doria hiyo inalenga kutathmini hali ya ukame katika mito hiyo, kiwango cha maji katika mabwawa, hali ya uzalishaji katika vituo hivyo, na kutathmini hatua za kuchukua kukabiliana na hali hiyo.

Waziri Makamba ameshuhudia mtiririko hafifu katika Mto Ruaha na kukauka vya mito midogo inayochangia katika mtiririko wa mto Ruaha na katika bwawa dogo la Kidatu. Hali hiyo imesababishwa na ukame mkali unaotokana na kutonyesha mvua katika maeneo yanayolisha mito hiyo na pia matumizi mabaya ya rasilimali-maji na uharibifu wa mazingira katika maeneo husika.

Pamoja na kadhia hiyo, waziri ameliagiza shirika lisijiingize kwenye kukodi mitambo ya dharura kutokana na historia mbaya ya mitambo ya aina hiyo kuwa na gharama kubwa kwa Serikali na kughubikwa na utata mwingi.

Badala yake, amelielekeza Shirika kuhakikisha kwamba linaongeza miradi mipya ya uzalishaji umeme kwa njia ya upepo na jua ambayo inaweza kutekelezwa ndani ya mwaka mmoja ili mwakani katika kipindi kama hiki cha umeme taifa lisikabiliwe tena na uhaba wa umeme.

Send this to a friend