Waziri Masauni amuonya Zumaridi, asema kanisa lake halijasajiliwa

0
47

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema Serikali itazichukuliwa hatua taasisi zote za kidini ikiwemo taasisi inayoendeshwa na Diana Bundala maarufu ‘Zumaridi’ ambazo zinajiendesha kinyume na tamaduni za Kitanzania.

Akizunguma katika kikao kati yake na viongozi wa mashirikisho na mabaraza ya kidini, amesema miongoni mwa taasisi hizo ni zile ambazo hazijasajiliwa likiwemo kanisa la Zumaridi.

“Zipo tasisi ambazo zinaibuka kama huyo Zumaridi, hajasajiliwa. Ametoka huko anajiita yeyeni kiongozi wa dini. Utakuta wengine wanahamisisha mapenzi ya jinsia moja, mwingine anajiita yeye ni Mungu, wanazungumza mambo ya ajabu ambayo hayawezi kukubalika,” ameonya Masauni.

Rostam aomba radhi kwa kauli yake aliyoitoa kwa mahakama

Amesema Serikali imekuwa ikichukua hatua kwa wote wanaokwenda kinyume na sheria kimaadili, mila na desturi pamoja na kueleza kwamba inapobainika kuna vikundi vya kidini vinavyotia shaka, ni vyema kutoa taarifa Ofisi ya Msajili ili kuiweka jamii katika hali ya usalama.

“Nichukue fursa hii kuwasihi viongozi wetu wa kiroho, kutoleta taharuki katika jamii kutokana na mafundisho mnayoyatoa yanaweza kutugawa katika kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili,” ameeleza.

Send this to a friend