Waziri Masauni: Sativa hatoi ushirikiano wa kutosha kwa polisi

0
103

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masaud amesema mwathirika wa vitendo vya utekaji, Edgar Edson Mwakabela (27) maarufu kama Sativa hatoi ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Polisi ili waliohusika kufanya tukio hilo waweze kuchukuliwa hatua.

Akizungumza katika mahojiano katika kipindi cha Good Morning, Waziri Masauni amemtaka Sativa kutoa ushirikiano na kueleza tukio hilo lililomsibu katika vyombo husika na si kwenye mitandao ya kijamii.

“Issue ya Sativa ni muhimu ili upelelezi wake uweze kwenda haraka, ni lazima yeye mwenyewe atoe ushirikiano kwa Jeshi la Polisi, ushirikiano wake bado ni mdogo katika kulisaidia Jeshi la Polisi kupata taarifa za yaliyomkuta,” amesema.

Ameongeza kuwa “wewe ndio ulioathirika, wewe ndio unayejua kwamba nimekamatwa na nani, yupoje baada ya kutoka hapo nikaenda wapi, eleza vyombo husika usieleze kwenye mitandao ya kijamii au Sativa aje wizarani kwangu aje anieleze mimi.”

Sativa alipotea Juni 23, mwaka huu majira ya saa 12 jioni na kupatikana katika Hifadhi ya Katavi akiwa amepigwa sana na hali yake ikiwa mbaya.

Send this to a friend