Waziri Mchengerwa aagiza watumishi watakaozuiliwa likizo zao walipwe

0
24

Waziri wa Nchi, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa likizo ni haki ya mtumishi kisheria hivyo hakuna haja ya kiongozi kuzuia haki hiyo isipokuwa kwa sababu maalum ambayo mtumishi husika atashirikishwa.

Mchengerwa ameagiza kiongozi anapotaka kuzuia likizo ya mtumishi kufuata taratibu ambazo ni pamoja na kuzungumza na mtumishi anayetaka kuchukua likizo na pia amlipe gharama za kuzuia likizo au kumsogezea mbele muda wa kuchukua likizo hiyo.

Amewataka viongozi kuwa na utamaduni wa kusoma nyaraka mbalimbali za kiutumishi ili kujua sheria na taratibu zitakazowaongoza pale wanapotaka kutoa matamko yanayozuia stahiki za mtumishi.

Amewataka viongozi kutotumia lugha za vitisho au vyeo vyao kwani wakifanya hivyo na kuzuia likizo, mtumishi anaweza asifanye kazi.

Send this to a friend