Waziri Mkuu aagiza baba anayedaiwa kumlawiti mwanaye akamatwe

0
25

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella kwa kushirikiana na Kamanda wa Polisi mkoani humo wahakikishe wanamfikisha katika vyombo vya sheria baba mzazi wa mwanafunzi wa darasa la pili (7) mkazi wa Kata ya Sokoni One mtaa wa Lonovono jijini Arusha anayetuhumiwa kumlawiti mtoto wake.

Ametoa agizo hilo leo Februari 17, 2023 baada ya kusambaa kwa taarifa kupitia vyombo vya habari vikimuonesha mtoto huyo anayedaiwa kufanyia vitendo vya ukatili na baba yake mzazi na kuagiza mtoto huyo atafutwe na kupatiwa huduma ya matibabu kwa haraka.

Waziri Mkuu amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan haitofumbia macho vitendo vya ukatili kwa watoto na kuitaka jamii kushirikiana katika kupiga vita vitendo hivyo pamoja na kutowaficha wale wote wanaohusika na unyanyasaji huo.

ZBC yaomba radhi kwa tamthilia iliyoonesha wapenzi wakiwa kitandani

Amesema katika siku za hivi karibuni kumeibuka tabia ya baadhi ya wazazi, walezi na wanajamii kuwafanyia watoto vitendo vya ukatili ikiwemo ulawiti, hivyo kuwasababishia maumivu makali pamoja na msongo wa mawazo hali inayowafanya baadhi yao kushindwa kuendelea na masomo. “Serikali haitosita kumchukulia hatua mzazi au mtu yeyote atakayebainika kufanya vitendo hivi vya ukatili.”

“Kumeibuka wimbi la ukatili wa kuwafanyia vitendo vya hovyo watoto wetu kwenye maeneo mbalimbali nchini, hivyo fanyeni uchunguzi na kubaini wanaohusika na vitendo hivyo. Wakuu wa Mikoa, Makamanda wa Polisi pamoja na Maafisa wa Ustawi wa Jamii hakikisheni mnawasaka watu wote wenye tabia hizo na kuwachukulia hatua,” amesisitiza.

Send this to a friend