Waziri Mkuu aagiza ngo’mbe kuvishwa hereni za kielektroniki

0
57

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kurudisha utaratibu wa kuiwekea hereni za kielektroniki kwa ajili ya utambuzi na udhibiti wa uingizwaji wa mifugo kutoka nje ya nchi bila vibali.

Amesema hayo Jumanne Mei 02, 2023 alipotembelea maonesho ya wadau wa mifugo na uvuvi yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge, jijini Dodoma.

“Wizara iliingiza mfumo wa kuvisha hereni. Hereni ya kielektroniki inaonesha tarehe aliyozaliwa, yuko maeneo gani na maendeleo yake. Ilikuwa na kasoro tukarekebisha, sasa wizara rudisha ule utaratibu.

Lakini wekeni vikao na wadau, utaratibu unarudi kwa sura ipi, sura ile iwe ni sura inayomwezesha mfugaji kuona kama kuna umuhimu wa kuweka alama ili kubainisha ng’ombe wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania,” amesema.

Ajira milioni 14 kutoweka ndani ya miaka mitano ijayo

Aidha, amesema mifugo mingi inayotoka nje inatumia rasilimali za Tanzania ikiwemo malisho ya mifugo ambayo iko mahususi kwa ajili ya mifugo iliyopo nchini na kupelekea bajeti kutokidhi mahitaji ya mifugo.

Hata hivyo Waziri Mkuu ameisisitiza wizara ya mifugo kuandaa utaratibu rafiki na utakaomwezesha mfugaji kumudu gharama za hereni kwa ajili ya mifugo nchini.

Send this to a friend