Waziri Mkuu aagiza shule zifundishe zaidi kuhusu Mwalimu Nyerere

0
18

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuandaa utaratibu utakaosaidia vijana kujifunza na kumfahamu zaidi hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuanzia shule za msingi, hadi vyuo vikuu.

Ameyasema hayo leo Mei 6, 2023 kwenye kongamano la kumbukizi ya miaka 101 ya Hayati Mwalimu Nyerere lililofanyika katika ukumbi wa Chimwaga, Chuo Kikuu cha Dodoma akimuakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mkuu amesema baadhi ya mambo ambayo vijana wanapaswa kurithishwa ni kuyafahamu maisha ya Mwalimu Nyerere hasa baada ya kustaafu uongozi wa nchi na siasa za majukwaani, kutambua juhudi zake katika harakati za kuleta amani na kufanikisha ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na bara la Afrika.

Mwanasiasa afungwa kwa njama za kuiba figo

“Miongoni mwa urithi huo ambao tungependa kizazi chetu kiufahamu ni pamoja na kuwa na uwezo wa kumfahamu na kumuelezea Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni nani katika historia ya Tanzania; kuzielewa na kuzitambua juhudi za zake katika kuimarisha ustawi wa Tanzania hususan kupitia falsafa yake ya kutokomeza maadui watatu yaani ujinga, umaskini na maradhi” amesema.

Send this to a friend