Waziri Mkuu amshukuru Rais kwa kumteua Naibu Waziri Mkuu

0
54

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiongezea nguvu Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kumteua Dkt. Dotto Biteko kuwa Naibu Waziri Mkuu ili waweze kusimamia na kuratibu shughuli za Serikali kwa pamoja.

Ameyasema hayo leo Septemba 02, 2023 wakati akimkaribisha rasmi Naibu Waziri Mkuu katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu zilizopo Magogoni jijini Dar es Salaam na kuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake.

“Kwa niaba yenu, Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu tunakukaribisha sana hapa katika ofisi yetu na tunakupongeza kwa kuaminiwa na Mheshimiwa Rais kupewa jukumu kubwa la Naibu Waziri Mkuu kwa lengo la kusimamia shughuli za Serikali. Nakuhakikishia kwamba una timu imara ambayo inatoa ushirikiano wakato wote,” amesema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kumuamini na kumteua kushika wadhifa huo, huku akiahidi kufanya kazi kwa ushirikiano.

Send this to a friend