Waziri Mkuu amwalika Rais wa CAF mechi ya Simba na Yanga

0
45

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuomba Rais wa CAF, Patrice Motsepe na wanachama wa CAF kuhudhuria katika mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga itakayofanyika Agosti 13 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa mkoani Dar es Salaam.

Ameyasema hayo katika Mkutano wa 44 wa Shirikisho la Soka (CAF) uliofanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mashirikisho kutoka nchi za Afrika na wadau wa michezo.

“Ningetamani tarehe 13 Agosti, 2022 muwepo hapa nchini Tanzania ili kushuhudia hali inavyokuwa pale miamba hiyo ya soko inapokutana katika moja ya mechi kubwa ya watani wa jadi (derby) na yenye msisimko mkubwa barani Afrika katika mechi ya ngao ya hisani,” amesema

TFF yawashtaki Manara na Eng. Hersi

Aidha Waziri Mkuu ameipongeza shirikisho kwa kuunga mkono soka la vijana na wanawake na kubainisha kuwa Tanzania iko tayari kuimarisha uhusiano wake na FIFA pamoja na wanachama wake wa CAF.

Mbali na hilo, amesema Tanzania inajivunia kuwa miongoni mwa nchi tatu kutoka Afrika kufuzu (kwa timu ya wanawake chini ya miaka 17 – Serengeti girls) kuliwakilisha bara la Afrika kwenye machuano ya kombe la Dunia itakayofanyika Oktoba mwaka huu nchini India.

Send this to a friend