Waziri Mkuu atoa siku saba TARURA, DAWASA kukamilisha barabara ya Muhimbili

0
44

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amempa siku saba Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Dar es Salaam, Godfrey Mikinga na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Usafi wa Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingiza (DAWASA), Lydia Ndibalema kukamilisha kipande cha barabara ya Mariki kinachoingia geti kuu la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kiwango cha lami.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo Julai 24, 2023 alipofanya ziara ya kushitukiza kukagua barabara hiyo.

Hata hivyo, barabara hiyo ambayo ilibomolewa kwa urefu wa mita 60 kupisha matengenezo ya bomba la maji machafu ilipaswa kuwa imekamilika mwishoni wa mwezi wa sita mwaka huu.

Waziri Mkuu amewaagiza watendaji hao kufanya kazi usiku na mchana ili kuepusha adha kwa wagonjwa na wanafamilia wanaoitumia barabara hiyo kuelekea hospitalini hapo.

Send this to a friend