Waziri Mkuu awataka wahandisi kutekeleza miradi kwa ubora unaoendana na thamani ya fedha

0
24

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wahandisi wote nchini wazingatie miiko na maadili ya taalum hiyo ikiwemo kutekeleza miradi ya ujenzi kwa ubora unaoendana na thamani ya fedha halisi iliyotolewa.

Ameyasena hayo leo kwenye Kongamano la Kimataifa la 14 la Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), jijini Arusha.

“Sote tunatambua kwamba wapo wachache katika taaluma yenu ya uhandisi ambao wanaichafua kwa kufanya matendo ambayo ni kinyume na taaluma lakini pia ni kinyume na maadili.”

Matendo hayo ni pamoja na rushwa, ubadhilifu, na ukosefu wa weledi. Hii si tu kwamba inachafua taaluma ya uhandisi, bali pia inaharibu taswira ya nchi,” amesema.

Aidha, Waziri Mkuu ameiagiza Bodi ya usajili wa Wahandisi isimamie maadili ya kihandisi na makampuni ya kihandisi kwa mujibu wa sheria ili kulinda hadhi ya uhandisi nchini.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amezielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa na Usalama Barabarani kuhakikisha kuwa vizuizi na vituo vya ukaguzi vinazingatia usalama wa watumiaji na tahadhari zote za kiusalama.

“Wahandisi na wataalamu wetu mnao wajibu wa kuendelea kubuni na kupendekeza mifumo bora ya alama za barabarani, usimamizi wa miundombinu ya barabarana uwekaji wa vituo vya ukaguzi ili kupunguza ajali na madhara yake.”

Send this to a friend