Waziri Mkuu awataka watumishi wa umma kuzingatia maadili

0
43

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma kuondoa urasimu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili wananchi wapate huduma bora.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na watumishi wa umma katika ziara yake ya kikazi Manispaa ya Singida, ambapo amewataka watumishi kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia maadili ya kiutumishi, sheria, taratibu na kanuni wakati wote wanapotekeleza majukumu yao.

“Mtu akija mhudumie moja kwa moja, hizi njoo kesho zinakaribisha majadiliano nje ya utaratibu wa Serikali, kwa lugha nyepesi rushwa. Tusitengeneze haya mazingira.” amesema Majaliwa.

Aidha, Majaliwa amewataka watumishi hao kutambua makundi mbalimbali katika jamii yakiwemo ya wazee, wanawake na vijana ili wapange namna bora ya kuwahudumia.

Waziri Mkuu ametoa wito pia kwa watendaji wa halmashauri kufanya tathmini ya maeneo ya ukusanyaji wa mapato kabla ya kuwakabidhi mawakala kazi ya ukusanyaji.

Send this to a friend