Waziri Mkuu: Hatuwezi kutoa umiliki wa bandari kwa kampuni yoyote

0
24

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ndiyo iliyopewa mamlaka na haki ya umiliki wa maeneo yote ya bandari nchini, hivyo hakuna chombo chochote wala TPA ambayo ina uwezo wa kutoa umiliki huo kwa kampuni yoyote ile.

Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akitoa hotuba ya kuahirisha bunge leo Juni 28, 2023 ambapo ametolea ufafanuzi kuhusu uwekezaji wa kampuni ya DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vitaendelea kutekeleza majukumu yao katika maeneo ya mradi kama ilivyofanya katika kipindi cha miaka 22 cha mkataba na mwekezaji wa awali (TICTS) ambaye amemaliza muda wake Novemba, 2022.

Kada wa CCM, Balozi Karume awekwa chini ya uangalizi

Aidha, amewahakikishia wabunge na wananchi kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaendelea kusimamia masuala ya mapato serikalini kutoka kwa mwekezaji kwa mujibu wa sheria na taratibu za mikataba.

Kwa upande mwingine, Chama cha Wakala wa Meli Tanzania (TASAA) kimeunga mkono mpango wa Serikali wa kuleta uwekezaji wa kampuni ya DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam, kikisema kuwa uwekezaji huo utasaidia kuongeza ufanisi wa bandari na kukuza uchumi wa Tanzania.

Mwenyekiti wa TASAA, Daniel Mallongo, amesema  kuna changamoto kadhaa za ufanisi kwenye bandari ya Dar es Salaam zinazolikosesha taifa mapato ambazo zinatarajiwa kupatiwa ufumbuzi na uwekezaji wa DP World.

Send this to a friend